1 Samuel 4:11-16

11 aSanduku la Mungu likatekwa, na hao wana wawili wa Eli, Hofni na Finehasi, wakauawa.

Kifo Cha Eli

12 bSiku ile ile mtu mmoja wa kabila la Benyamini akakimbia kutoka kwenye uwanja wa vita na kwenda Shilo, nguo zake zikiwa zimeraruka na akiwa na mavumbi kichwani mwake. 13 cAlipofika, Eli alikuwa ameketi juu ya kiti chake kando ya barabara akiangalia, kwa sababu moyo wake ulikuwa na hofu kwa ajili ya Sanduku la Mungu. Mtu yule alipoingia mjini na kueleza kilichokuwa kimetokea, mji wote ukalia.

14Eli akasikia kelele za kilio, naye akauliza, “Ni nini maana ya makelele haya?”

Yule mtu akafanya haraka kwenda kwa Eli,
15wakati huu Eli alikuwa na miaka tisini na minane nayo macho yake yalikuwa yamepofuka na hakuweza kuona. 16 dAkamwambia Eli, “Mimi nimetoka vitani sasa hivi, nimekimbia kutoka huko leo hii.”

Eli akamuuliza, “Je, mwanangu, ni nini kimetokea huko?”

Copyright information for SwhKC